SIKILIZA WIMBO HUU KWA MAKINI
UTAKUSAIDIA, NA MUNGU ATAKUSAIDIA
Naomba Msamaha (wee naomba Baba)
Naomba msamaha (ee nisamehe Baba)
Naomba msamaha (oho Baba)
Kweli nimekosa (sitarudia tena)
Naomba msamaha (nisamehe Baba)
Naomba msamaha (nimemuua mke wangu Baba)
Naomba msamaha (wee nisamehe mimi)
Kweli Nimekosa (nimeua mume wangu mimi)
Naomba msamaha (wee naomba Baba Mimi)
Naomba msamaha (watoto wangu watabaki na nani wee)
Naomba msamaha (ee naomba Yesu wee)
Kweli Nimekosa (kweli nimekosa)
Najua ulikuwa una malengo mazuri
Ulikuwa bado unatamani kukaa na mke wako
Lakini tumaini limeondoka
Tumaini haliletwi na dawa
Tumaini linaletwa na Toba
Hakuna mzigo mzito kwenye maisha ya mtu kama dhambi
Umekwenda nje ya ndoa yako
Madhara unayo ndani ya mwili wako
Umemletea mke wako ambaye hakuwa nayo
Umemletea mme wako ambaye hakuwa nayo
Kwa nini useme nakimbilia arusha kwenda kupona
Kwa nini kwanza usikimbilie kwa Mungu kutubu
Kwa nini kwanza usikimbilie kwa mke wako
Kumwambia nisamehe nimekuletea jidudu
Nisamehe mme wangu nimekuletea jidudu
Nisamehe Mungu nimekutenda dhambi
Naomba uniponye, mbona atakuponya
Nataka niwaambie watanzania
Toba ina nguvu kuliko kitu chochote
Ndo mana wakina petro walimwambia Yesu
Pepo zinatutii, wagonjwa wanapona
Yesu akasema hayo sio yakushangilia
Shangilieni majina yenu yameandikwa Mbinguni
Moyo wangu ukaniuma nikasikia
vijana siku moja wanasema
sasa hivi ni kufanya uzinzi kwenda mbele
Na ndo mana wengine bado wanaendelea kuumwa
Tatizo ni dhambi ndani ya mioyo ya watu
Mimi ngoja niwaambie Abiud
Mungu anawapenda na bado tumaini lipo
Akarudisha tena uhai wenu
Akabadilisha dawa maana ndiye yeye aliyeiumba
Jambo la msinigi la kumwambia Mungu
Ukiwa katika chumba chako sasa hivi
Upo kwenye ofisi yako mwambie Nimekosa
Halafu mwambie Yesu niponye kwa damu yako
Na mimi namwambia Yesu akuponyee
ili uendelee kuwaona watoto wako
Ili uendelee kumuona mke wako
Ili uendelee kuwaona wazazi wako
Nami nakwombea nasema upone kwa jina la Yesu
Naomba Msamaha (wee naomba Baba)
Naomba msamaha (ee nisamehe Baba)
Naomba msamaha (oho Baba)
Kweli nimekosa (sitarudia tena)
Naomba msamaha (nisamehe Baba)
Naomba msamaha (nimemuua mke wangu Baba)
Naomba msamaha (ehe nisamehe mimi)
Kweli Nimekosa (nimeua mume wangu mimi)
Naomba msamaha (ee naomba Baba Mimi)
Naomba msamaha (watoto wangu watabaki na nani wee)
Naomba msamaha (wee naomba Yesu mii)
Kweli Nimekosa (kweli nimekosa)
Nataka niponywe (naomba niponywe Baba)
Nataka niponywe (Baba nataka niponywe)
Nataka niponywe (Wee niponywe)
Nataka niponywe (kwa jina kwa jina la Yesu)
Nataka niponywe (Nirudi kazini kwangu)
Nataka niponywe (niendelee kuona watoto wangu mke wangu)
Nataka niponywe (wee niponywe baba)
Nataka kikombe (Nataka kikombe)
Nataka kikombe (nataka kikombe nataka kikombe)
Nataka kikombe (wee kikombe)
Nataka kikombe (Nataka kikombe)
Nataka kikombe (mm Nataka kikombe)
Nataka kikombe(wee kikombe)
Nataka mafuta (Wee sio ya chupa)
Nataka mafuta (wee Nataka mafuta)
Nataka mafuta (wee mafuta)
Nataka mafuta (Weewe mafuta)
Nataka mafuta (Baba nataka mafuta)
Nataka mafuta (Wee mafuta)
Nataka maji (wee nataka maji)
Nataka maji (mimi ninataka maji)
Nataka maji (Wee ninywe Abiud)
Nataka maji (Nisione kiu ya dhambi)
Natangaza kikombe cha kwanza ni toba
Добавил: Frol4ic